Bayport

Bayport

VODACOM

VODACOM

Tuesday, June 11, 2013

FIKA DIDA CLASSIC BOUTIQUE KINONDONI STUDIO...

Rangi za kucha za SALLY HANSEN SALON "Nail Lacquer" kutoka Marekani. Zipo za kila aina hapa ni chache tu kwenye picha. Hizi ni rangi za kucha original kabisa....


Pia katika mzigo toka Marekani kuna Bikini za kila aina njoo uone...


Kuna PERFUME babkubwa toka Marekani, zenye uwezo wa kukaa muda mrefu zaidi zikipuliziwa katika nguo. Nazo zipo aina mbalimbali kwa bei poa kabisa....

Mzigo ni wa uhakika na wote safari hii toka Marekani njoo uone magauniya kila aina....


Monday, June 10, 2013

MSANII WA BONGO MOVIE “KASH” AFARIKI DUNIA

Habari zilizotufikia ni kwamba msanii wa filamu nchini Jaji Khamis maarufu kama (Kashi) aliyewahi kutamba na michezo ya ITV enzi zile akiwa na wasanii kama mzee masinde, samson na wengine katika mchezo wa TAMU CHUNGU na mingine mingi Amefariki dunia mchana huu katika hosptali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.


Nae MZEE MASINDE ambaye alikuwa nae katika kundi moja akiwa kama kiongozi wake amesema kashi ni msanii huyo ambaye alikuwa mpiganaji na kwa hakika ni pigo kubwa katika tasnia hiyo.

 Tunaona SANAA ya Tanzania bado inaendelea kukumbwa na majanga, ikiwa si muda mrefu umepita tangu Mama mzazi wa DUDE, msanii wa HipHop ALBERT MANGWAIR na Mume wa malkia wa mipasho Khadija Kopa JAFARI ALLY wafariki dunia.

Mungu ailaze roho ya marehemu Jaji Khamis (Kashi)
mahali pema peponi Amina.


 

TUZO ZA KTMA 2013 ZILIVYOKUA J’MOSI...

HATIMAYE kitendawili cha nani kavuna nini katika kinyang’anyiro Kilimanjaro Tanzania Music Awards KTMA 2013, kilipata jibu usiku wa jumamosi, ambapo kategori zote za mchakato huo zilipata washindi, huku wasanii Kala Jeremiah na Ommy Dimpoz wakifunika kwa upande wa muziki wa kizazi kipya.



 
Kala Jeremiah akimaliza kwa kutwaa tuzo tatu za Wimbo Bora wa Mwaka (Dear God), Msanii Bora wa Hip Hop na ile ya Mtunzi Bora Bora wa Hip Hop, huku akiipoteza ya Wimbo Bora wa Mwaka wa Hip Hop(Dear God) iliyochukuliwa na Nay wa Mitego kuptia wimbo Nasema Nao.



 
Kwa upande wa Dimpoz, nyota pekee aliyekuwa akiwania tuzo saba katika kinyang’anyiro hicho, alipata tuzo tatu za Wimbo Bora wa Bongo Pop (Me and You feat Vanessa Mdee), kibao kilichompa pia tuzo ya Wimbo Bora wa Ushirikiano.



 
Dimpoz akapokea tuzo ya tatu ya Video Bora ya Mwaka kupitia kibao cha Baadae,huku akiangukia pua katika kategori nne za Wimbo Bora wa Mwaka, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume, Msanii Bora wa Mwaka wa Kiume – Bongo Flava na Mtunzi Bora wa Mashairi – Bongo Flava.
 
Katika namna iliyowavutia wengi, Dimpoz aliitoa kwa Vanessa Mdee moja ya tuzo mbili alizoshinda kupitia kibao alichomshirikisha cha Me and You kwa, tukio lililotafsiriwa kama ‘kumpoza’ binti huyo aliyeangukia pua katika kategori ya Msanii Bora Anayechipukia, ambayo ilienda kwa Ali Nipishe.



 
Bendi ya Mashujaa waliibuka kidedea zaidi katika mchakato huo, baada ya kujizolea tuzo tano, kupitia mbili za bendi (Wimbo Bora wa Bendi – Risasi Kidole) na Bendi Bora ya Mwaka, huku ikitwaa tatu za wasanii wake, ambao ni Chalz Baba aliyetwaa mbili za Mtunzi Bora wa Mashairi – Bendi na Msanii Bora wa Kiume – Bendi.
 
Pia rapa wake Ferguson aliibuka kidedea katika kategori ya Rappa Bora wa Bendi, alikowabwaga Greyson Semsekwa, J4, Jonico Flower na Sauti ya Radi.
 
Ukiondoa washindi wa Kategori 35, KTMA 2013 ilitoa tuzo mbili maalum; moja ya All of Fame ilitwaliwa na kundi la Kilimanjaro Band ‘Wana Njenje’ ambayo ilipokelewa na Waziri Ali, huku ile ya Individual All of Fame ikinyakuliwa na nyota wa muziki wa zamani marehemu Salum Abdallah na kupokelewa na mwanaye.
 


Thursday, June 6, 2013

POLE SANA KHADIJA KOPA KWA KUFIWA NA MUME

Mume wa Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki, Khadija Omar Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.  




Marehemu alikuwa anasumbuliwa na matatizo katika mfumo wa upumuaji na mpaka mauti yanamfika alikuwa amelazwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMEN.


ONE B a.k.a MOKO BIASHARA AKIWA NA M 2 THE P

M 2 THE P akiwa na namba nyingine toka Times Fm 100.5 MokoBiashara mwite ONE B host wa THE TRENDING AFRICA "Washa Hukoo" mchana huu Moro kwenye msiba muda mfupi baada ya M 2 THE P kuwasili kutoa heshima zake za mwisho kwa aliyekua mshikaji wake wa karibu na walikua wote mpaka mauti yanamfika marehemu ALBERT MANGWAIR. Karibu nyumbanii Tanzania M 2 THE P


TUKIWA MSIBANI MORO MCHANA HUU

Moro kwenye msiba wa kijana mwenzetu, mwana sanaa, mwana hiphop aliyekubalika na wengi na Mkali wa FREESTYLES ndugu ALBERT MANGWAIR


Jinsi alivyokua anakubalika inaonekana wazi kutokana na uwingi wa watu waliojitokeza kushiriki shughuli za msiba kuanzia mapokezi yake kule airport Dar es salaam mpaka huku nyumbani Morogoro ambako ndio leo atapumzishwa katika nyumba yake ya milele. Mungu amlaze mahali pema peponi....


Nawaona Ommy Dimpozi akiwa na Diamond Platnumz


Vanessa Mdee mwenye njano na Dyna katikati tukiwa msibani


M 2 THE P NDIO AMEFIKA MORO MSIBANI SASAHIVI

Huyu ndiye M 2 THE P ambae kwa wengi walikua hawamfahamu vizuri na mchana huu ndio ameingia Morogoro hapa ni nyumbani kwasasa bado watu wanaaga mwili wa Ngwair. Karibu nyumbani 
M 2 THE P


Hapa katika Picha nyingine


Wednesday, June 5, 2013

BIG BROTHER "THE CHASE" WIKI HII....

Baada ya Kenya na Uganda kufungua mlango wa kurudisha washirki nyumbani toka shindano kubwa Afrika la BIG BROTHER wiki hii Tanzania tupo kwenye hati hati ya kumpokea mshiriki wetu wa kike FEZA KESSY kutoka katika jumba hilo ambalo maisha yake sehemu kubwa ni starehe...


Watanzania tuonyeshe uzalendo kwa kumpigia kura FEZA KESSY kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi. Andika neno FEZA kisha tuma kwenda namba 15456 au tembelea website ya BBA kwa ku click hapa  VOTE FOR FEZA 


HAYA NI MAJIBU KUA NGWAIR ALIPENDWA KIASI GANI.... TAZAMA MAPOKEZI YA MWILI WAKE

Mashabiki wengi wa aliyekua Mkali wa Freestyles, Mwanachemba, Cowboy, Cowbama, Albert Mangwair walijitokeza leo katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere kupokea mwili wa Ngwair aliyefariki tarehe 28 mwezi wa 5 huko Afrika ya kusini.


Katika umati huo uliojitokeza wengi walikua ni mashabiki, marafiki, ndugu, wasanii wenzie na wengi walioshirrikiana na Albert Mangwair katika tasnia ya muziki kwa njia moja ama nyingine. Watangazaji na Ma-Dj pia walikuwepo katika umati huo ulioashiria UPENDO mkubwa kwa kuondokewa na msanii mwenye uwezo mkubwa kwenye game.


Mtayarishaji wa muziki P-FUNK mwenye mchango mkubwa katika career ya Ngwair akiwa sambamba na TID katika mapokezi ya mwili wa mwenzetu...

Katika sura za majonzi, Namuona Profesa Jay, Lady Jay Dee, P-Funk na wengine wakiwa pamoja katika kipindi hiki kigumu




Mungu amlaze mahala pema peponi AMINA.

Kila mmoja anasikia uchungu kwa aina yake na kila mtu ana njia yake ya kufikisha ujumbe wa kile anachojisikia. Atakumbukwa sana Ngwair hususani kwa uweo wake wa kufanya FREESTYLES


Watu walijitokeza kwa wingi sana, japo kushuhudia ujio wa mwili wa marehemu Albert Magwair


Sunday, June 2, 2013

KILLING A WEEK-END SOMEWHERE....

Hamna hata maelezo mengi, tazama tu picha zina jieleza week-end ilikuaje. I hope ya kwako ilikua poa pia


Kabla hujatumia shurti kujaribu kwanza kidogo, mwanamke Jacuzzini/ pembeni lina sehemu ya muziki unaoga huku unakula ngoma zako swaafi


Hapa ndani ya Steam Shower au sauna


Na hapa ndipo palee sasa wapumzika....!!! Wikiendi ya maana


Feeling the water, povu smelling so good. Hata stress zote kapuni hapa




Hiki ni kiti maalumu kwa kufanya massage, una-set tu hapo maeneo gani ya mwili, kiti kinafanya mambo yake 







The living room wengie husema seating room au sebule, what an apartment 



Bedroom




Upande mwngine wa sitting room, the sofa set



Big Brother Africa yafanya nichelewe kulala



The Bath-room







Nawatakia week end njema wapendwa 



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...